Zifahamu Kampuni Za Mabasi Zinazoongoza Kwa Huduma Bora Nchini Tanzania.
Hivi ulishawahi kukaa na kujiuliza ni kampuni ipi ya mabas inayoongoza kwa kutoa huduma bora nchini Tanzania? Kama bado hebu jiulize leo hii na ikiwa tayari ulishawahi kujiuliza ulipata jibu gani?
Twende pamoja hapa, Tanzania ni miongoni mwa nchini zenye idadi kubwa ya wamiliki wa mabas ya kusafirisha abiria. Hata hivyo zipo aina mbalimbali za mabasi nchini Tanzania ikiwemo Yutong, Zhong, Golden Dragon, Eicher, Scania na nyingine nyingi.
Kila aina ya basi ina ubora na sifa zake ambazo aina nyingine haina, baadhi ya kampuni za mabasi ya kusafirisha abiria zilizopo nchini Tanzania ni pamoja na Tahmeed, Shabiby, Tashrif , Kimbinyiko, Abc Upper Class, Esther Luxury Coach, Lim Safari, Ratco, Arusha Express, Kapricon, Raqeeb, Msawa, Hajees, Kandahar, Mtei Express, Shaibaba, Simba Mtoto, Bm na nyingine nyingi.
Kabla ya kuendelea zaidi inakubidi ufahamu kuwa vigezo kadhaa hutumika kufahamu ni kampuni zipi zinaongoza kwa huduma bora ikiwa ni pamoja na vigezo kama vile huduma bora kwa wateja, Mfumo bora wa kukata ticket mtandaoni, Uimara wa gari mwanzo hadi mwisho wa safari zake , Kuzingatia ratiba ya safari, bei rafiki kwa abiria pamoja na muonekano mzuri.
Kufuatia vigezo tajwa kampuni hizi zifuatazo ndio vinara wa huduma bora nchini Tanzania nazo ni kama vile :-
1.Tahmeed Tahmeed ni kampuni yenye huduma nzuri sana na kinachoipa upekee wa huduma zake ni muonekano mzuri wa basi zao , seat nzuri za luxury na pia uimara wa basi zao kuanzia mwanzo hadi mwisho wa safari. Japokuwa mfumo wao wa kukata ticket mtandaoni hauvutii sana lakini ni mfumo rahisi ambao hauchanganyi akili ya mtumiaji. Huduma Ya Kusambaziwa Seafood Inapatikana Hapa
2. Shabiby Katika kampuni ambazo zimejipanga katika utoaji wa huduma za usafirishaji wa abiria basi Shabiby ni miongoni mwa kampuni hizo. Hii kampuni unaweza kusema inafaa kuwa namba moja , unajua kwanini? Kwanza Shabiby ina gari za kutosha, zenye muonekano mzuri na imara, mfumo wake wa ticket mtandaoni ni rahisi na wenye kuvutia pia. Lakini kama haitoshi kitengo chake Cha huduma kwa wateja kipo vizuri sana. Huduma yao ya kusafirisha mizigo ( parcel) ipo vizuri sana pia.
Hata bei za nauli katika kampuni ya Shabiby ni rafiki kwa abiria isipokuwa bei ya luxury coach kidogo ipo juu lakini ubora wa huduma za kwenye bus za luxury inaendana na bei.
3. Abood Bus Hii kampuni bwana! ukiziona bus zao kwa nje unaweza kusema ni ndogo, fupi na bus za kawaida, lakini kiukweli ukiingia ndani ya bus hizi kama abiria huwezi kusahau kamwe raha utakayoipata. Ukiachana na uwepo wa sehemu za kuchajia simu , choo na WiFi, comfortable seat kwenye bus za abood zitakufanya uione raha ya safari yako na kukufanya usitamani kufika unapokwenda.
Inabidi ufahamu kuwa idadi ya gari za kutosha katika kampuni ya Abood kunafanya kampuni hii kuwa bora, lakini pia uimara wa basi zao kuanzia mwanzo hadi mwisho wa safari zake kunaiongezea kampuni hii kuwa bora. Umeuona mfumo wao wa kukata ticket mtandaoni? kiukweli ni mfumo rahisi sana wenye muonekano mzuri . Usikose Mtumba Quality Tsh 5,000 Tuu
Bus zote hupata ajali, lakini cha ajabu ni kuwa ajali za kampuni ya abood mara nyingine huwapelekea watu kidogo kuwa na hofu wanaposafiri na bus za abood.
4. Bm Coach Hizi bus bwana hhhh, ni nzuri sana na ukiziona tuu zinashawishi kusafiri nazo, unajua kwanini? Kwanza ni muonekano mzuri wa bus za hii kampuni, bei nafuu ya nauli na huduma nzuri za customer care. Safari zilizopangiliwa Fresh Seafood Wanapatikana Hapa kunaiongezea thamani kampuni hii . Hata hivyo ukiangalia online ticket system yao kuna upekee utauona, mfano orodha ya safari, nambari za simu muhimu na viungo vingi muhimu kwaajili ya mawasiliano.
5. Kimbinyiko Mfumo wao wa kukata ticket mtandaoni ukiingia tuu utakupelekea wewe kufahamu kuwa kweli hii kampuni ipo serious na utoaji wa huduma za usafirishaji. Bus za hii kampuni kuna muda hupata damage katika safari lakini uzuri ni kuwa sio damage za kufanya abiria wapate kero .
Kinachovutia zaidi katika Kampuni hii ni huduma yao ya kusafirisha mizigo au parcel kiukweli wamejipanga sana , unapoenda kupokea mzigo wako ofisi za kampuni ya Kimbinyiko utafurahishwa na namna wanavyopangilia mizigo store kwao , yaani huwezi kupata tabu kuutafuta mzigo wako.
Hata hivyo hakuna kampuni inazingatia ratiba kama kampuni ya Kimbinyiko, hata hivyo huduma ya vinywaji ndani ya bus za Kimbinyiko inadhihirisha ubinaadmu wao kwa abiria .
6. Buti La Zungu Safari kutoka Dar es Salaam hadi mtwara inatosha kuipa thamani kampuni hii. Kuwa na mfumo wake binafsi wa kukata ticket mtandaoni kunaiongezea thamani kampuni za Buti la zungu. Hizi bus bwana zinaenda kwa ratiba sana kitu kinachopelekea abiria wengi kuipenda.
7. Kidia One Express Rangi yake ya blue kunafanya gari hizi zionekane nzuri sana. Kidia One Express sio kampuni kongwe sanaa lakini mfumo wake wa ticket mtandaoni kunapelekea kampuni hii kuwa maarufu na bora hapa nchini Tanzania.
Hizi ni kampuni chache tuu , kampuni zipo nyingi lakini vigezo vilivyoainishwa baadhi ya kampuni hazina, kwako mdau unafikiri kampuni ipi ni namba moja kwa huduma bora za usafirishaji wa abiria nchini Tanzania? Tuandikie maoni yako Instagram account ya modealer online tv.