Header Ads

Historia ya Rihanna in Swahili language.

Modealer Online TV

 Jina kamili anaitwa Robyn Rihanna Fenty, Alizaliwa February 20, 1988  Saint Michael na kukulia Bridgen town , Barbados huko Jamaica.

Ni mtoto wa accountant Monica na Warehouse supervisor Ronald Fenty. Na amebahatika kuwa na Kaka wawili, Rorrey na Rajad Fenty, na anao dada zake wadogo pia na Kaka wadogo wa upande wa baba yake ambao Kila mmoja ana mama yake.

Rihanna alikulia katika bungalow lenye vyumba vitatu tuu na akiwa na umri mdogo alisaidiana na baba yake kuuza nguo mtaani .

Maisha yake ya utotoni hayakuwa na furaha kamwe, kutokana na maradhi ya kichwa yaliyokuwa yakimsumbua Sana, na maisha yake ya utotoni yalimuathiri zaidi kutokana na baba yake kuwa mlevi na kukubuhu katika matumizi ya cocaine, Vitendo hivi vilisababisha wazazi wake kutengana kindoa na sio kuachana kabisa. Baba mzazi wa Rihanna aliongoza katika kumpiga mama Rihanna na muda wote huo Rihanna alikuwa msuluhishi wa ugomvi.

Akiwa na umri wa miaka 14 tuu wazazi wake waliachana moja kwa moja na hapo afya yake ilianza kuimarika .

          (  Maisha ya masomo)

Rihanna alisomea Charles F .Broome memorial primary school na Combermere School , Ambapo huko alikutana na kusoma pamoja na wacheza cricket Chris Jordan na Carlos Bathwaite.

    Kitu pekee usichokijua : Rihanna ni army cadet in a Sub -military programme, na baadae kuwa mwanamuziki.



Kipaji chake kiligunduliwa na kuendelezwa na na producer wa mziki aitwae Evan Rogers huko U.S.A na alimualika u.s.a kwenda kurekodi demo tapes.

Baada ya kusaini mkataba na Def Jam mwaka 2005 alitambulika rasmi na kutoa albam mbili .moja aliita Music of the sun (2005) na nyingine  A girl like me(2006) .

              

2 comments:

Note: only a member of this blog may post a comment.

Powered by Blogger.