VIOJA VYA KABILA LA OVAHIMBA
Kabila la Ovahaimba na Ovazimba ni makabila maarufu sana nchini Namibia Katika mkoa wa kunene na omusati Namibia kaskazini .
Ni kabila lenye idadi ya watu 50,000 . Shughuli kuu ya kiuchumi ni pamoja na ufugaji yaani pastoralism na livestock keeping.
Mgawanyo wa Kazi huzingatia jinsi pamoja na rika . Wanawake shughuli kuu ni pamoja na kukamua maziwa katika mifugo , lakini wanaume hujishughulisha na uwindaji.
Katika kitu ambacho ni tofauti na makabila mengine duniani ni swala la uchumba na ndoa .
Kabila hili wanawake huolewa kwa kuchaguliwa wachumba na wazazi wao wa kiume ndipo huolewa.
Kabila hili ni kabila lenye kupenda urembo na kwa miaka kadhaa wamekuwa mstari wa mbele katika kudumisha urembo wa asili kwa kufanya make-up ya asili.
Hutumia butterfat, Omuzimba scrub na ochre . Mchanganyiko huu huunda rangi nyekundu katika ngozi zao . Rangi nyekundu katika ngozi zao ni imani kuu yenye maana ya dunia na damu .
Pamoja na hayo yote rangi nyekundu huwasaidia kulinda ngozi zao dhidi ya jua na kuumwa na wadudu wenye sumu.
Kabila hili linaongoza kwa kupenda mapenzi na huwa ni utaratibu kwao kuwakaribisha wageni kwa kuwapa penzi .
Habari picha ya warembo wa kabila la Ovahaimba wakijipamba kwa katika kundi .
Nice story
ReplyDelete