Header Ads

MATUKIO MAKUU TANZANIA

 Matukio Makuu katika siku ya leo nchini Tanzania. Yapo matukio ya kufurahisha na kuhuzunisha.

Haya hapa matukio Makuu matatu ya nchini Tanzania yaliyovuma sana katika mitandao ya kijamii.

1. Kifo Cha Panya Magawa .

Panya Magawa ni maarufu sana kwa ushujaa na uwezo wake wa kusaidia vikosi mbalimbali vya ulinzi katika uteguaji wa vilipuzi (mabomu ) .

Ni kama ajabu kwa kiumbe panya kuwa na uwezo huu wa ajabu , lakini kwa Panya Magawa kutoka Tanzania ni jambo jepesi sana . Kitu pekee ambacho ni Cha huzuni na simanzi ni pale mapema leo hii tarehe 11/01/2022 vyombo mbalimbali vya habari viliporipoti kifo Cha Panya Magawa.
Taarifa kutoka shirika la herorat zilithibitisha kutokea kwa kifo hiki kupitia ukurasa wao wa instagram.

Panya Magawa enzi za uhai wake alifuzu katika mafunzo mbalimbali na pia kupokea tuzo mbalimbali.

2. Ajali iliyoua watu 14 leo .


Mapema leo hii tarehe 11/01/2022 vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania viliripoti kutokea kwa ajali mbaya iliyohusisha gari mbili . Gari moja ni hiace ya abiria na nyingine gari ya serikali iliyokuwa imebeba waandishi wa habari wa mkoani Mwanza .

Gari hizi ziligongana uso kwa uso katika eneo la Chumve  Wilaya ya Busega mkoani Simiyu . Mganga mkuu mfawidhi wa hospital moja huko Simiyu anathibitisha kupokea maiti 11 na majeruhi tisa na kisha majeruhi watatu kufariki baadae.
Waandishi wa habari walikuwa wakielekea katika majukumu yao ya kikazi.

3. Rais Samia Suluhu Hassan kuzindua kiwanda Cha nguo Zanzibar.

Habari kubwa nyingine ni hii kutoka Tanzania visiwani.
Mhe Rais Samia Suluhu Hassan amezindua kiwanda Cha nguo Cha Basra Textile Mills Ltd mapema leo hii tarehe 11/01/2022 .






No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

Powered by Blogger.