TISA KUGOMBEA USPIKA
Katibu wa Bunge la Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania Ndugu Nenelwa Mwahambi amethibitisha kuwa hadi kufikia leo saa kumi jioni majina ya jumla ya wagombea tisa (09) yaliwasilishwa na kukidhi na kukidhi matakwa ya kisheria kwaajili ya uchaguzi wa kiti Cha spika .
Uchaguzi wa spika wa Bunge unatarajiwa kufanyika tarehe 01/02/2022 . Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma katibu wa Bunge amesema kuwa miongoni mwa wagombea hao nane (08) sio wabunge na mmoja ni mbunge .
Wagombea hao ni pamoja na Abdullah Mohammed Said (NRA) , Mhandisi Aivan Jackson Maganza (TLP) , David Daud Mwaijojela , Georges Gabriel Mwiru (SAU) , Maimuna Said Kassim (ADC) , Ndonge Said Ndonge (AAFP), Saidoun Abrahamani Khatib (DP) na mwisho ni Mheshimiwa Dkt Tulia Ackson (Member of parliament) .
Post a Comment