Header Ads

SUKAMAHELA KITOVU CHA TANZANIA.

 

 

SUKAMAHELA : Huwenda ikawa si mara yako ya kwanza kusikia hili eneo . Pia huwenda ikawa ulishasikia hili eneo lakini leo tunakufungulia ufahamu wako .

SUKAMAHELA ni kijiji kilichopo kati ya mkoa wa Dodoma na Singida.Eneo lenye mawe mengi sana makubwa na maumbo tofautitofauti . Sukamahela eneo ambalo baadhi ya wataalamu wa jiografia hulitumia sana katika taaluma zao . Eneo la sukamahela kwa miaka mingi limekuwa likitajwa kuwa ndio katika ya Tanzania ( Center) 


Katika eneo hili lipo jabali kubwa ambapo hapo ndio ipo point iliyowekwa kama alama kuwa ndipo katikati ya nchi ya Tanzania.

Yapo mengi sana ya kujivunia lakini na hili pia ni miongoni mwa mambo ya kujivunia. Kujua katikati ya  nchi si jambo jepesi linahitaji utaalamu wa juu kabisa. Inaelezwa kuwa umbali kutoka mashariki, magharibi , kaskazini ukiwa eneo hili ni sawa .


     Jee unatamani kufahamu jambo gani         jingine? Baki na sisi kila siku upate           kufahamu mengi zaidi katika dunia .




No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

Powered by Blogger.