Waziri Mkuu Wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Azungumzia Swala La Bandari .
Dodoma: Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mhe. Kassim Majaliwa amesema kuwa serikali ya itahakikisha kuwa mikataba ya utekelezaji wa makubaliano ya uendeshaji wa maeneo ya bandari nchini kati ya nchi ya Tanzania na dubai kupitia kampuni ya dp world inazingatia maslahi ya taifa na kuleta manufaa.
" Kuhusu umiliki wa bandari, nilihakikishie bunge lako na wananchi kwa ujumla kwamba, kupitia sheria ya bandari ya mwaka 2004 , Tanzania Port Authority ( TPA ) imekasimiwa haki ya kuwa mmiliki wa maeneo yote ya bandari nchini na haina uwezo wa kutoa umiliki huo kwa kampuni nyingine". Kassim Majaliwa .
Waziri mkuu Kassim Majaliwa ameyasema haya leo june 28 akiwa bungeni mjini Dodoma akiahirisha vikao vya bunge la jamhuri ya Muungano Wa Tanzania .