Mbegu Za Apple Unaweza Kufa Ukizila Sana
Image Credit/ Marco Pixabay.Kamwe hukatazwi kula matunda aina ya apple, kula apple ni kitu kizuri lakini kula mbegu zilizopo kwenye apple ndio kitu kibaya ambacho kamwe hushauriwi.
Tafiti zilizofanywa kuhusu matunda yenye sumu ndani yake zimebaini kuwa ulaji wa mbegu zilizopo katika apple kwa kiwango kikubwa kunaweza kupelekea kifo chako.
Mbegu za apple zina idadi kubwa ya cyanogenic glycosides, hata hivyo kula mbegu za apple moja tuu haitoshi kufanya upate madhara makubwa au kifo , madhara unaweza kuyapata pindi utakapotafuna mbegu hizo kwa kiasi kikubwa zaidi.