Arusha: Chama cha upinzani nchini Tanzania, Chadema leo February 27, 2024 kimefanya maandamano yake ya amani kushinikiza serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan chini ya Chama cha mapinduzi CCM kufanya mabadiliko ya katiba mpya na pia kupunguza makali ya ugumu wa maisha.
Aidha maandamano ya chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho akiwemo mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa chama hicho. Maandamano ya Chadema jijini Arusha ni hitimisho la maandamano ya takribani siku 33 tangu kuanza kwa maandamano ndani ya majiji kuanzia January 24.
Pichani ni ujumbe wa waandamanaji wa Chadema jijini Arusha " Ni haki yetu kupata maisha nafuu " , " We want free and fair election" .