Grand Mosque Algeria Washika Namba Tatu Kidunia

Msikiti Mkubwa Wajengwa Algeria Grand Mosque Washika Namba Tatu Kidunia . 

Grand Mosque Algeria

Algeria: Nchini Algeria kumejengwa msikiti mkubwa wa kisasa ambao kidunia unakadiriwa kushika nafasi ya tatu kwa ukubwa, baada ya msikiti wa Makkah na ule wa Madina basi unaofuata kwa ukubwa ni msikiti huu wa Algeria.

Djamaa El Djazair ni jina uliopewa msikiti huu wenye ukubwa wa eneo wa Hekta 27.75 sawa na acres 70 . Msikiti wa Djamaa El Djazair unatajwa kuwa na uwezo wa kubeba waumini 120,000 katika ibada.  

Mpaka sasa gharama zilizotumika katika kujenga msikiti huu ni takribani dollar 898 million, chini ya Chinese construction company msikiti huu umekidhi malengo na nia ya Rais Abdelmajid ambae alidhamiria kujengwa kwa msikiti huu tangu 2010 .  

Hata hivyo msikiti wa Djamaa El Djazair kwasasa umekuwa kivutio kikubwa cha wageni wanaotembelea nchi ya Algeria, lakini hata hivyo msikiti huu unatarajiwa kutumiwa kwaajili ya ibada za usiku katika mwezi mtukufu wa ramadhan mwezi ujao.