Sheria Ya Kuwahasi Wabakaji Madagascar.
Nchi ya Madagascar imepitisha sheria ya kuruhusu kuwahasi wanaume wanaobaka. Aidha sheria hiyo inaruhusu wabakaji kuhasiwa kwa kutumia dawa au upasuaji.
Sheria hiyo inawalenga zaidi wale wanaokutwa na hatia za makosa ya ubakaji, hata hivyo wanaharakati wa nchini Madagascar wanaiunga mkono sheria hii kukomesha utamaduni wa kesi za ubakaji , huku wanaharakati wa kimataifa wakiipinga sheria hii kwa kuiita ni kunyume na ubinaadamu. Mchongo Umetiki 2024
Mpaka sasa sheria hiyo inasuburi kusainiwa na Rais Andry Rajoelina wa Madagascar.