Rais Samia Suluhu Na Papa Francis Wazungumza Vatican Italy Leo .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na kiongozi wa kidini Papa Francis huko Vatican Italy.
Hata hivyo kiini cha mazungumzo yao hakijajulikana, nini wanajadili bado haijulikani lakini viongozi hao wamekutana na kuzungumza mambo mbalimbali huko Vatican.
Rais Samia Suluhu Hassan anakutana na Papa Francis ikiwa ni siku kadhaa tangu kiongozi huyo kutamka waziwazi kuwa ndoa za mapenzi ya jinsia moja zinapaswa kubarikiwa, lakini hata hivyo Papa Francis baada ya kupata ukosoaji na upingamizi mkali kutoka kwa watu mbalimbali duniani aliongeza kwa kusema kuwa wote wanaopinga ndoa hizo ni wanafiki.
Ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan huko Vatican inatarajiwa kudumisha amani , umoja na mshikamano kati ya Tanzania na Italy pamoja na Vatican.