BIASHARA YA KAROTI ILIVYOBADILI MAISHA YAKE
Baada ya kumaliza chuo na kukosa fursa ya ajira Deborah , mhitimu wa masomo ya chuo kikuu shahada ya sayansi za jamii, mwaka 2020 chuo kikuu Cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam. Deborah alirudi nyumbani kwao Dodoma bila matumaini . Pita nayo story nzima hapo chini .
Deborah ni binti wa umri wa miaka 25 kutoka katika familia ya bibi na Bwana james kingai . Mtoto wa nne katika familia ya watoto sita . Baada ya kusoma kwa tabu kutokana na hali ngumu ya uchumi wa nyumbani hatimae alifika chuo kikuu na mwaka 2020 kuhitimu masomo bila uhakika wa ajira .
"Hata ile siku ya mahafali sikuwa na furaha kabisa kila nikiwaza kuhusu nini nitafanya kupata kipato changu ......lakini nilikuwa na wazo..." Deborah anaieleza timu ya modealer Online Tv akiwa ofisini kwake.
Nilirudi Dodoma na kuongea na mama kuhusu wazo langu lakini hakuwa na uwezo wa kunisaidia kwa wakati ule . Sikupenda kuwa mzigo wa familia .
Siku moja niliamka na kwenda soko la mboga pale sabasaba na kuhoji wakina mama wafanyabiashara ile na nilijua nianzie wapi .
Nilichukua carrot za 5,000 na kurudi nyumbani kisha nilizipanga nje kujaribu na sikuuza hata moja . Siku ya pili mchana nilizitembeza mtaani na mpaka saa sita hivi sikubaki na hata moja.
Hivyo ndivyo nilivyoanza na kisha sasa nilifungua genge na kusogeza huduma karibu na jirani zangu kuwapunguzia safari za kwenda mbali kununua mboga. Mwezi mmoja tuu nilizoeleka sana na kupendwa .
Nilivumilia sana na kuongeza juhudi na Ili kukuza biashara yangu nikaanza kuajiri kijana mmoja ambae alikuwa akipitisha biashara mtaani na mimi nilibaki gengeni na baada ya miezi sita hivi nikopa pesa na kuongeza kidogo na faida yangu na kumnunulia yule kijana pikipiki ya kupitia wateja wangu na kuwaachia bidhaa.
Jee mpaka sasa deborah una kipi Cha kujivunia na biashara yako?
"Najivunia kumiliki biashara kubwa zilizotokana na biashara hii ya carrot.
Kwa sasa Nina mgahawa mkubwa , bajaji tatu kiwanja na pia nauza mtumba pale sokoni sabasaba japo bado ninaishi kwa mama.
Hayo ni maelezo ya deborah james na wewe jee unasubiri nini?
Tafadhali kwa kuikosa video kamili vifaa vyetu vilikuwa duni wakati wa mazungumzo.
Piga simu namba 0759634586 kisha tueleze ulipo na unafanya nini na kipi unatamani kuwaeleza wengine kupitia modealer online Tv Instagram, facebook , twitter na modealer blog .
Nice
ReplyDelete