Header Ads

KUGOMA KWA FACEBOOK, INSTAGRAM & WHATSAPP DUNIA NZIMA


Mapema hapo jana na leo pia mamilioni ya watumiaji wa mitandao ya kijamii ya facebook, instagram na whatsapp wamekuwa katika   changamoto ya KUGOMA kwa mitandao tajwa ghafla bila kutarajia na kusababisha mijadala na taharuki ya ghafla .

Hakuna hata mmoja anayefahamu kuhusu nini tatizo haswa . kupitia mtandao wa twitter watu mbalimbali wanaendelea kuchangia mawazo na maoni  yao juu ya like wanachokiamini kuhusu taharuki hii.


Aidha watu mbalimbali wamekuwa wakijiuliza swali kuwa kwanini facebook, instagram na whatsapp tuu na si mitandao mingine?  Hata hivyo baadhi ya watu wamekuwa wakisema kuwa hasara kubwa imemfika mmiliki wa mitandao tajwa Mark zuckerberg ingawaje bado haijathibitishwa ni hasara gani na kiwango kipi .

Katika nchi za magharibi yaani Europe na America tatizo lilianza mapema sana kama inavyozungumzwa na  wengi kupitia ukurasa za twitter .


Bado mpaka sasa  haijafahamika ni lini haswa huduma za mitandao tajwa zitakuwa sawa kama hapo awali .

Tutakufahamisha zaidi kuhusu mwenendo wa urudishwaji wa huduma kadri taarifa zitakavyopatikana .




No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

Powered by Blogger.