KWANINI NDOA NYINGI HUVUNJIKA ? SABABU NI MIGOGORO
Hakika hili ni swali gumu sana kulijibu Maana kila ndoa au uhusiano fulani huwa kwa sababu zake . Sababu zilizovunja ndoa fulani huweza kutofautiana na sababu za ndoa au uhusiano mwengine .
Kwasasa kumekuwa na vilio vingi sana juu ya ndoa na uhusiano wa watu fulani kuvunjika mapema sana haswa kwa vijana. Kuliona hili leo hii ningependa kujadili na umma wa walimwengu wote .
Je ulishawahi kupitia kipindi Cha ndoa yako kuvunjika? Kama jibu ni ndio ulijiuliza ni kwanini ilitokea? Kama jibu ni hapana basi hapa ni mahala pakujifunza Ili isikukute.
Ndoa ni nini?
Ndoa ni Muungano Kati ya mwanamke na mwanaume waliokulia katika mazingira tofauti na sasa wanaungana kuishi pamoja katika maisha ya mume na mke . Mapenzi ya dhati, huruma na nidhamu ndio silaha kuu ya kuwawezesha kuishi pamoja .
Mapenzi ya dhati, huruma na nidhamu vitakapokosekana basi hiyo si ndoa tena. Swali ni jee kwanini mapenzi ya dhati, huruma na nidhamu vikosekane.?
Hizi hapa ni baadhi ya sababu kuu :-
1. Kupenda kurudiarudia kosa
Hii ni sababu kubwa sana na ndio mzizi mkuu wa migogoro mingi kwa wapenzi na Wana ndoa . Ni kawaida kukosea maana hakuna kiumbe kikamilifu hapa ulimwenguni . Kumbuka kuwa hakuna kosa dogo na "Kosa sio kosa ,bali kurudia kosa ndio kosa". Unapofanya kosa na mwenza wako akakukosoa basi hakikisha unaweka kichwani mwako kua ukitenda hicho kitu unamkera. Sasa utakaporudia rudia ndivyo na yeye anavyozidi kuchukia mwisho ni kupunguza mapenzi yake ya dhati kwako .
2. Kupenda matumizi makubwa yasiyoendana na kipato Cha mwenza wako.
Hukatazwi kupenda matumizi makubwa ya pesa kwenye vile uvipendavyo , lakini zingatia sana hali halisi ya kiuchumi aliyonayo mwenza wako. Kupenda matumizi makubwa yasiyoendana na kipato Cha mwenza wako kutamfanya ajihisi kero , huna malengo na yeye na pia kumuondolea furaha ya kuwa na wewe maana umeshakuwa adui kwake.
3. Ubishi na jeuri
Kuwa katika ndoa au uhusiano haimaanishi kuwa kila jambo ukubaliane nalo . Hata hivyo hakuna sababu ya kushikamana na ubishi katika yale ambayo hakuna sababu ya kuyapinga .
4. Matumizi ya lugha kandamizi, ubabe na yenye matusi pamoja na kashfa .
5. Uvivu na matumizi mabaya ya rasilimali .
Ahsante Sana kwa kusoma na Kupitia blog yetu na karibu sana katika muendelezo wa mada za mahusiano na ndoa bila kusahau habari za magazetini, michezo ,watu mashuhuri , historia za miji , mitindo ,urembo , Afya na biashara .
Tuandikie kwenye upende wa comment .
Post a Comment