Header Ads

UHABA WA AJIRA NI JANGA LA DUNIA?


 

Kwanza kabisa elewa kuwa kuna tofauti Kati ya uhaba na ukosefu . Pia kuna tofauti Kati ya Kazi na ajira .   Twende  sambamba.
Uhaba tafsiri yake ni kwamba kitu kilikuwepo mwanzo kwa wingi lakini sasa kimetoweka au kipo lakini kwa kiasi hafifu.
Ukosefu maana yake ni kitu au rasilimali ambayo haipo sasa na pia mwanzo hakikuwepo  kabisa . (Maana zisizo rasmi)
Ajira ni nafasi ya uwajibikaji yenye kumpa mtu kipato katika muda mahususi baada ya kukidhi katika viwango fulani vya kitaaluma 
Kazi ni kitu chochote ambacho mtu hufanya muda wowote , mahali popote na kupokea malipo yoyote bila kuzingatia kiwango Cha taaluma.
Dunia ni sayari ambayo binadamu huishi kuanzia karne nyingi zilizopita.
Swali : je dunia ipo katika upungufu au ukosefu wa ajira ? Na Kwanini?
Huwenda majibu yakawa ni tofauti lakini kwa kifupi dunia sasa ipo katika upungufu wa ajira . Twendeni  sambamba tuelewe .
Miongo kadhaa iliyopita walimwengu walishuhudia soko la ajira likipungua kidogo kidogo bila kujua sababu dhahiri na hata kama walifahamu maarifa yalizidi mbio .
Watu wengi Sana waliamini kuwa baada ya masomo ajira ni hatua inayofuata na ukweli ni kwamba  ilikuwa hivyo hapo awali lakini sasa zama zimebadilika haswa bara la Africa. Sababu ni nini? 
1. Mapinduzi ya teknolojia ; Mapinduzi au maendeleo ya sayansi na teknolojia ni sababu ya kwanza na kubwa katika kuzizika ajira nyingi sana .  Makumi na mamia ya ajira sasa hivi imekuwa gumzo kwani ni wazo hazina soko na nafasi . Mfano ajira za postal station  zimekuwa chache sana kutokana na maendeleo ya njia za mawasiliano ambapo simu ndio kila kitu na hivyo matumizi ya barua ni duni sana .
Mfano wa pili ni ajira telecommunications engineering haswa katika ujenzi wa minara kasi na nafasi ni chache kutokana na kupungua kwa uhitaji wa minara  satellite  sasa ndio kila kitu .
2. Kubadilika kwa soko la ajira duniani ; Hii ni sababu ya pili ya kupungua kwa ajira duniani haswa katika nchi za Africa . Hitaji la soko la ajira kwasasa limewatupa mkono wengi na kupoteza ajira za wengi . Soko la ajira la sasa hivi halihitaji sana mtu kukaa Ofisini kutekeleza majukumu.
Katika nchi za ulaya na America saa za mtu kukaa Ofisini zimepunguzwa , ambapo sasa hivi mtu huweza kukaa nyumbani kwake na kufanya majukumu ya ofisi . Hata hivyo soko la ajira la sasa ni soko mtandao , ambapo kwasasa platforms na social media ni chanzo kikubwa sana Cha kipato ambapo wengi huwekeza katika media na platforms na kutoa ajira kwa wachache wenye taaluma za marketing kupitia mitandao ya kijamii na ambao hawana ujuzi huachwa kwenye mataa  . 


Ukweli nikwamba sababu ni nyingi sana lakini hizo mbili ni mizizi mikuu na nyingine ni ndogo ndogo mfano kuwekeza nguvu kubwa katika mfumo wa elimu wenye nadharia nyingi , Kutothamini vipaji na ubunifu , sera dhaifu za mataifa ya Africa, Umaskini na kukosa wataalamu wakutosha katika rasilimali watu .
 Kifupi ni kwamba swala la upungufu wa ajira mizizi mikubwa ipo katika mataifa ya Africa lakini ulaya idadi ya wasio ajira ni ndogo sana kutokana na uelewa wao mzuri wa kuzalisha fursa za mtandaoni na kuzifanyia Kazi . Mfano  fursa za mtandaoni kama blogging , youtuber , instagramer , money exchange kama forex trading na nyingine nyingi kama photography , website designing .

Nini kifanyike ? Wewe kama kijana nini ufanye kujipa kipato au ubaki kusema ajira hakuna? Andika comment yako kisha fuatilia chapisho lijalo la mbinu za kijikwamua na kujipa fursa na uhuru wa kipato 







No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

Powered by Blogger.