Header Ads

FAIDA ZA KULA PANZI

 


Unashauriwa kujifunza mambo mapya kila siku na kama ukishindwa basi tulia utafunza na kufahamishwa na modealer online Tv.

Bila shaka panzi unamfahamu lakini kuhusu swala la kuliwa kwake na faida zake katika mwili na maisha ya binadamu huwenda ikawa ni jambo jipya kwako . Inaelezwa kuwa panzi ni kiumbe chenye faida nyingi kwako binadamu lakini ni vile wengi hawafahamu faida hizo .

Mwaka 2019 idara (taasisi) ya biology chuo kikuu Cha Mexico maarufu kama Biology institute of the national autonomou university of Mexico (UNAM ) ilifanya tafiti kuhusu faida za panzi kwa binadamu.


Tafiti ya chuo ilikuja na majibu kuwa panzi ni kiumbe chenye faida nyingi sana yaani zisizohesabika katika maisha yangu mimi na wewe msomaji wa website hii tunaekupenda

Zifuatazo ni faida za ulaji wa panzi kwa binadamu nazo ni pamoja na :-

         .Huongeza vitamini katika mwili wa                  binadamu ; Kwa mujibu wa UNAM panzi wanaongeza kwa haraka vitamin A, B, na C katika miili ya binadamu. Hii hutokana na tabia ya panzi kupendelea kula majani zaidi ya chakula kingine chochote.

          . Huongeza protein haraka ; UNAM inawataja panzi kuwa kichocheo Cha haraka katika kuongeza protein kwenye miili ya binadamu. Inaelezwa kuwa panzi huongeza protein haraka kuliko maziwa, nyama ya kuku au Samaki. 

           . Huongeza nguvu mwilini; Inaelezwa kuwa panzi huongeza nguvu katika mwili wa mlaji mara mbili ya ngano na vyakula vingine vya carbohydrates kama mhogo nk.

              .Wanawingi wa fibers , Magnesium, Calcium pamoja na Zinc ; Inaelezwa kuwa panzi pia ni wenye wingi wa madini tajwa . Madini ambayo yatamusuru binadamu katika matatizo ya afya ya uzazi ikiwa ni pamoja na upungufu wa nguvu za kiume .

              . Hawana sumu wala kemikali zozote zile ; hata hivyo UNAM inaeleza dunia kuwa panzi kamwe hawana sumu wala kemikali zozote zile hivyo ni salama katika ulaji .

               . Husaidia usagaji wa chakula tumboni na pia ni rahisi kuwameza; UNAM imethibitisha kuwa panzi husaidia usagaji wa chakula tumboni kwa binadamu na pia huwa rahisi sana katika kuwameza kipindi cha ulaji hivyo kamwe hawaathiri umio wa chakula . 

Ungependa kufahamu nchi zinazoongoza ulaji wa panzi kama chakula muhimu kwako?

Linapokuja swala la nchi ambazo tayari raia wake wanatumia panzi kama chakula muhimu sana kwao basi hizi nchi mbili ni kinara wa mataifa mengine.

1. Mexico : Kwa zaidi ya miongo kadhaa iliyopita nchi ya Mexico inaongoza katika ulaji na upatikanaji wa masoko yanayouza panzi kama kitoweo au chakula muhimu sana kwao. Majimbo na maeneo kama Morelos, Guerrero na mexico city ni mashuhuri katika uuzaji na utumiaji wa panzi kama chakula muhimu kwao .

2. Thailand : Thailand ni Taifa la pili katika kinara matumizi ya panzi kama chakula muhimu chenye faida nyingi mwilini upishi wa panzi Thailand ni tofauti na ule wa Mexico . Thailand panzi hukaangwa na kukaushwa kisha huongezwa viongo vingine kuongeza mahadhi au ladha .

Ungetamani kujua kitu gani kingine? Ungana nasi hapa katika kipindi chetu Cha report za siku na fahamu session kila siku .

Ahsante sana kwa kusoma habari hii .

Ukiwa na habari zozote za ukweli na uhakika, matukio katika eneo lako , michezo na burudani karibu kwa kuwasiliana nasi social media zote kwa jina la Modealer Online TV . Instagram account , facebook page, Twitter , linkedin, telegram channel & Pinterest. 



No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

Powered by Blogger.