MUSSA ZUNGU ASHINDA
Nchini Tanzania Mussa Zungu ashinda kiti cha unaibu spika wa Bunge la Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania leo hii .
Summary:
Mbunge wa Ilala , Mussa Zungu ametangazwa kuwa mshindi wa kiti Cha naibu spika wa Bunge la Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania baada ya wabunge kumpigia kura . Mussa Zungu amepata ushindi huo sawa na 98.33% . Katika uchaguzi huo kura zilizoharibika ni mbili tuu .Huku wabunge 296 wakipiga kura za ndiyo na wabunge watatu tuu kura za hapana . Mussa Zungu ametangazwa kuwa mshindi kwa tiketi ya chama chake Cha CCM.
Uchaguzi huu umefanyika wiki kadhaa baada ya uchaguzi wa kumpata spika wa Bunge la Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania ambapo Mhe. Tulia Ackson alishinda kiti cha kuwa spika wa Bunge la Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania. Chaguzi hizi zimeibuka baada ya Ndugai kujiuzulu nafasi ya kuwa spika wa Bunge la Tanzania.
Ahsante kuwa msomaji wa habari zetu .
Post a Comment