Header Ads

GSM KUJITOA UDHAMINI LIGI YA NBC PREMIER

 


Leo tarehe 07 February 2022 , uongozi wa kampuni ya GSM unatangaza rasmi kujitoa kwenye nafasi ya kuwa mdhamini  mwenza wa ligi kuu  ya NBC PREMIER . Sababu kubwa iliyofanya hata kufikia maamuzi haya ni kwa TFF na bodi ya ligi kushindwa kutekeleza baadhi ya vipengele vya kimkataba kama pande hizi mbili zilivyokubaliana .

Ikumbukwe kuwa GSM ilishawishika sana na TFF pamoja na bodi ya ligi na kuridhia kuwa mdhamini mwenza wa ligi kuu Ili kukuza sekta ya hii ya mpira wa miguu hapa nchini pamoja na michezo kwa ujumla lakini hili halikwenda kama ilivyokusudiwa .

Haya hayajakuwa maamuzi rahisi kwa kampuni ya GSM kwani tunatambua kuwa vipo baadhi ya vilabu vya mpira vitakavyoumizwa pamoja na wadau mbalimbali na hatua hii na wala haikuwa dhamira yetu kufikia uamuzi huu mgumu.

GSM inapenda kuwashukuru TFF , bodi ya ligi , vilabu vyote pamoja na wadau wote kwa kuwa sehemu ya kuendeleza sekta ya michezo hapa nchini. 

Tunapenda kuwatakia kila la kheri wadau wote wa mpira , mashabiki na wanamichezo wote katika kuendeleza mchezo huu pendwa na tunawashukuru wote kwa kutuamini.

Milango ya GSM bado ipo wazi kwa wadau wa michezo kuendelea kushirikiana nasi katika kuendeleza tasniya hii na michezo mingine kwa manufaa ya Taifa letu la Tanzania .

Vilevile kwa niaba ya Ghalib  Said Mohamed ambaye ni mwenyekiti na mjumbe wa kamati ya ushindi ya timu ya Taifa (Taifa Stars) analeta kwenu Taarifa kuwa amefanya maamuzi magumu ya kujiuzulu nafasi ya mwenyekiti pamoja na mjumbe wa kamati hiyo kuanzia leo . Anawashukuru sana viongozi wote katika nafasi mbalimbali kwa kumuamini na kumpa nafasi hii . Na yeye anawatakia wadau wote kila la kheri.

           ALLAN CHONJO .

AFISA BIASHARA MKUU MAKAMPUNI YA GSM .


Picha https://www.instagram.com/p/CZreqMPqT3s/?utm_medium=copy_link

   Hapo juu ni taarifa ya GSM baada ya CHONJO kufanya mazungumzo na waandishi wa habari leo tarehe 07 February . Nini maoni yako?

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

Powered by Blogger.