VITA UKRAINE vs RUSSIA
Breaking news : UKRAINE vs RUSSIA
Habari za muda huu popote ulipo ni matumaini yetu kuwa upo salama , mwenye amani na furaha nyingi na kubwa .
Vyombo mbalimbali vya habari duniani kote vinaendelea kuripoti habari za uvamizi wa Russia katika nchi ya Ukraine na kusababisha hofu , woga na uharibifu wa vitu mbalimbali na pia vifo vya raia na wanajeshi wa Taifa la Ukraine.
Habari zinaeleza kuwa mpaka sasa madhara yaliyojitokeza kwa upande wa Ukraine ni makubwa sana . Vifo vya raia na wanajeshi wapatao 317 vimeripotiwa mapema leo hii na Rais Volodymyr Zolenskyy wa Taifa la Ukraine. Hata hivyo Kambi zipatazo 70 za kijeshi zimelipuliwa na ndege 11 aina ya airbus zimeharibiwa huko nchini Ukraine.
Mbali na hivyo Rais wa Russia Vladimir Putin hana mpango wowote wa kusitisha adhma yake ya Vita dhidi ya Ukraine.
Taarifa zinasema kuwa Rais Volodymyr Zolenskyy wa Ukraine ameweka kizuizi kwa wanaume wa nchi yake kusafiri na badala yake wajiingize katika kuitetea nchi yao , uhuru wao na ardhi yao .
Mpaka sasa miundombinu kadhaa ya barabara na madaraja vimeharibiwa nchini Ukraine. Huku majengo mbalimbali katika maeneo ya Umma yakiendelea kulipuliwa kwa mabomu . Hata hivyo taarifa zinasema kuwa vikosi vya majeshi ya uvamizi kutoka Russia vinazidi kujiingiza katika miji mingine ya nchi ya Ukraine hali inayoongeza wasiwasi wa raia na mali zao.
Waume wote kuanzia umri wa miaka 18-60 nchini Ukraine wametakiwa kujiingiza katika kuvikabili vikosi vya majeshi ya uvamizi kutoka Russia bila woga . Rais Volodymyr Zolenskyy ametoa wito kwa wenye uwezo wa mapambano kuingia katika kuvikabili vikosi vya majeshi ya Russia kutetea uhuru wao na ardhi yao .
Hata hivyo serikali ya UKRAINE imetoa tovuti maalumu kwa lengo la watu dunia kote kupata habari za kweli juu ya kinachoendelea . Hatua hii imefikiwa Ili kuepusha propaganda katika tukio la wao kuvamiwa na Taifa la Russia na kusababisha uharibifu mkubwa kwao .
Ahsante kwa kuwa sehemu ya wasomaji wetu . Endelea kuwa karibu nasi kwa habari za kitaifa, kimataifa, michezo na burudani.
Post a Comment