Header Ads

AN 255 . NDEGE YA UKRAINE ILIYOHARIBIWA VIBAYA

 

                Antonov airlift cargo story 

Mnamo mwaka 1980 Rezo Chorkviani aliiunda ndege ya An 255 Mriya . An 255 ndege iliyoweka rekodi ya kuwa ndege kubwa ya mizigo duniani kuliko ndege zote.

 Inaelezwa kuwa AN 255 ilitengenezwa mmoja tuu na ilikuwa na uwezo wa kubeba tani zaidi ya 650 za mizigo . AN 255  ndege ya kimkakati katika ubebaji wa mizigo tuu.

Kipindi ndege ya AN 255 inaundwa Taifa la Ukraine lilikuwa katika Umoja wa Soviet Union. Ndege hii designed na  Antonov Design Bureau in Soviet Ukraine. 

       Kuruka kwa AN 255  mara ya kwanza

Mnamo mwaka 1988 ndege hii kubwa na ya kipekee iliruka kwa mara ya kwanza katika maonesho ya ndege ramsi kwaajili ya kuanza shughuli zake za ubebaji wa mizigo.

Ndege hii iliwavutia wengi sana kipindi cha kupaa na hata kutua kwake kutokana na rangi zake nzuri za bendera ya Ukraine . Baadhi ya watu walifikia hatua ya kukaa karibu na uwanja wa ndege kuweza kuiona ndege hii kipindi ikitua huko Ukraine.


Taifa la Ukraine lilijivunia sana kumiliki ndege hii na kuhisi fahari kubwa kuwa nayo , ikumbukwe kuwa Ukraine ilibaki na ndege hii baada ya Soviet Union kuvunjika . Ndege yenye mengi mazuri na kuvutia ilizidi kuibua furaha kwa Taifa la Ukraine kila kukicha . Muonekano wake wa ndani ulishangaza wengi sana kutokana na kuwa na ukumbi na vyumba vikubwa sana .

         Muonekano wa ndani AN 255 Mriya 

Mwisho wa uhai wa AN 255 airlift Cargo.

Huzuni na simanzi ni mwisho wa uhai wa AN 255 . Wakati vyombo mbalimbali vya habari duniani vikiendelea kuripoti kisa cha uvamizi wa Russia nchini Ukraine ndipo hapahapa habari za kuharibiwa vibaya kwa ndege hii zinapoanzia .

Habari kutoka uwanja wa mapambano huko Ukraine siku chache zilizopita zinaeleza kuwa ndege hii kubwa na kipekee dunia nzima ni kuwa imeharibiwa vibaya sana kutokana na makombora ya angani kutoka kwa vikosi mbalimbali vya mashambulizi kutoka Russia. Inaelezwa kuwa hii ni hasara kubwa sana kwa Taifa la Ukraine katika vita inayoendelea . Japo jitihada za mazungumzo ya amani zikiendelea kumaliza vita hivi.

Ukraine na raia wake na watu wengine duniani wameendelea kupigwa na butwaa kutokana na kuharibiwa kwa ndege hii kubwa ya mizigo duniani. Swali ni jee kwanini Russia wameamua kuharibu ndege hii? Kulikoni? . Bado uharibifu huko Ukraine ni mkubwa sana katika miundombinu ya barabara, viwanja vya ndege ,makazi ya raia na kambi mbalimbali za kijeshi.

Mamilionioni ya watu wamekimbia makazi yao kwa kuishi ukimbizini kuokoa uhai wao 

Muonekano wa AN 255 baada ya kuharibiwa


No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

Powered by Blogger.