Header Ads

PASTOR ABI ADELEKE APIGWA VIBOKO

                SOWETO - NIGERIA  

                     Pastor Abi Adeleke 

Summary : 

Wanaume watatu waliingia kanisani siku ya jumaapili na kuanza kumchapa wakimtuhumu kumpa ujauzito dada yao na kisha kukataa ujauzito huo . Ahadi ni kwamba kila jumaapili mchungaji Abi Adeleke ameahidiwa kupigwa na watu hao .

Mchungaji Abi Adeleke huko Soweto nchini Nigeria amejikuta katika wakati mgumu baada ya kupigwa na wanaume watatu akiwa katika mahubiri kanisani jumaapili iliyopita. 

Habari zinasema kuwa wanaume watatu waliingia kanisani siku ya jumaapili na kuanza kumpiga (kumchapa) mchungaji Abi Adeleke akiwa anahubiri  . Wanaume hao wamempiga Abi Adeleke kwa kosa la kumpa ujauzito dada yao na kisha mchungaji Abi Adeleke kukataa ujauzito huo na pia kukataa kuhudumia . 

Mchungaji Abi Adeleke kila mara amekuwa akikataa swala la kupima DNA . Hata hivyo wanaume hao wameahidi kumchapa mchungaji Abi Adeleke kila siku ya jumaapili. 

      Tafadhali tunakuhitaji sana , endelea kuwa karibu nasi . Kuwa sehemu ya wasomaji wetu kila siku. Ahsante.

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

Powered by Blogger.