Header Ads

DINOSAUR: WALIKUWA WAKITAGA MAYAI

 DINOSAUR WALIKUWA WAKITAGA MAYAI KAMA NDEGE  


DINOSAUR: Huwenda ikawa sio mara yako ya kwanza kusikia jina la viumbe hawa wakubwa wanaodhaniwa kuwepo katika dunia miaka million mingi iliyopita

Ni viumbe wenye umbo kubwa sana, uzito na nguvu nyingi sana. Tafiti nyingi zilifanywa na bado zinaendelea kufanywa kuhusu viumbe hawa (Dinosaur). Kwenye miaka ya 1820 tafiti ya kwanza ilifanywa juu ya viumbe hawa huko England na iligundulika kuwa Dinosaur walikuwa wakitag mayai na hivyo ni wazi kuwa walikuwa ni reptile. 


Hata hivyo mwaka 1859 yai la Dinosaur liligunduliwa huko ufaransa na Jean Jacques Poech . Haikuishia hapo tafiti na gunduzi  ziliendelea kufanywa mpaka kufikia 2022. 
Mwaka 2022 yai jingine la dinosaur liligunduliwa huko nchini India, na tafiti zilionyesha kuwa yai hilo halikuwa la kawaida. 

Timu ya watafiti kutoka katika chuo kikuu cha Delhi, Madhya Pradesh iligundua yai hilo ndani ya hifadhi ya Taifa ya Dinosaur Fossil iliyopo eneo la Dhar. 

Jambo pekee na la ajabu nikwamba mpaka leo hii bado imekuwa vigumu kugundulika ni aina gani ya dinosaur ambao walikuwa wakitaga mayai . 

   


No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

Powered by Blogger.