PRECISION AIR KUONDOKA NA ROHO 19
AJALI YA NDEGE SHIRIKA LA PRECISION AIR NDANI YA ZIWA VICTORIA 6/11/2022
Picha: Ndege ya shirika la Precision Air ikiwa katika maji ya ziwa Victoria baada ya kutua kutokana na ajali. Picha iliyopigwa 06/11/2022 ziwa Victoria Bukoba Tanzania.
Vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania mapema leo hii vimeripoti kutokea kwa ajali ya ndege shirika la Precision Air , ndege hiyo yenye usajili namba 5H-PWF, ATR42-500. ilikuwa inasafiri kutoka Dar es Salaam kwenda Bukoba majira ya 06:53 huku ikiwa na abiria 39 ( 38 watu wazima na 01 mtoto) pamoja na 04 wahudumu wa ndege pamoja na marubani , imepata ajali na kuanguka katika ziwa Victoria. Jitihada za uokoaji zimefanyika na mpaka kufikia saa moja kamili za jioni idadi ya waliofariki imefikia 19.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila amesema idadi ya Watu waliofariki kutokana na ajali ya ndege ya Precision Air iliyotokea asubuhi leo Ziwa Victoria wakati ikitua imefikia Watu 19 “Jitihada haizidi kudra ya Mungu”
Post a Comment