Australia Baba Wa Watoto Wawili Afariki Kwa Kuumwa Na Nyoka Mke Wake Akishuhudia
NCHINI AUSTRALIA BABA WA WATOTO WAWILI (2) AFARIKI DUNIA KWA KUUMWA NA NYOKA MBELE YA MKE WAKE .
AUSTRALIA: Baba mmoja amekufa kifo cha kusikitisha kutokana na kuumwa na nyoka mwenye sumu kali huko Queensland . Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 60 anadaiwa kuumwa mkono katika eneo la Lockyer Valley, takriban kilomita 50 kutoka Brisbane, kabla ya saa 10 asubuhi Jumamosi.
Hata hivyo ina ya nyoka huyo bado haijathibitishwa kulingana na ripoti ya aina za sumu za nyoka , lakini inaaminika kuwa huwenda nyoka huyo akawa ni Eastern Brown .
Jirani wa mwanamume huyo Michelle Vedredi aliiambia Courier Mail kuwa alipokea simu na jumbe kadhaa kutoka kwa familia na marafiki kufuatia mkasa huo. Lakini muda mchache baadae kabla ya mwanaume huyo kupata huduma za kitabibu alifariki duniani.
