Habari: Rais mstaafu wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete ameshinda tuzo ya kiongozi bora wa amani na usalama wa mwaka 2023 katika jarida la uongozi wa kiafrika 2023.
Mbali na Jakaya Mrisho Kikwete wengine walioshinda tuzo hii ni Rais William Ruto wa Kenya, Rais mstaafu wa Liberia George Weah kwa pamoja wameibuka kuwa washindi katika tuzo za kumi na mbili viongozi bora wa mwaka kwenye Jarida hilo la uongozi wa kiafrika kwa mwaka wa 2023 .
Aidha watatu hao wameibuka na ushindi kwenye vipengele vya kiongozi wa usalama wa mwaka, Mwafrika wa mwaka na Kiongozi wa kisiasa wa mwaka hii ni kutokana na matokeo ya kura ya mtandaoni ambayo ilionekana kuwa na ongezeko la 29% ya kura tofauti na mwaka uliopita.
Sherehe za utoaji wa tuzo hizo zimefanyika tarehe 15 mwezi march katika hafla ya kila mwaka ya tuzo za watu bora wa mwaka nchini Ethiopia mkuu wa Addis Ababa makao makuu ya umoja wa Africa yalipo. Aidha sherehe hizo zilizoandaliwa na ALM kwa ushirikiano na Tume ya forodha nchini Ethiopia zimeshuhudia uzinduzi wa toleo maalumu la POTY jarida la uongozi la Africa.
Mgeni rasmi waziri wa mapato wa nchini Ethiopia Aynalem Nigusie ndie aliyemkabidhi Dk Jakaya Kikwete tuzo yake ya ushindi, hata hivyo mgeni rasmi aliambatana na mwenyekiti wa Jarida La Uongozi Africa, Dk Ken Giami. Hata hivyo Dk Giami amesema na kusisitiza kuwa hatua kubwa na michango ya washindi katika uhai wa mwamko wa bara la Africa katika kuendesha maendeleo endelevu, ukuaji wa kiuchumi na utulivu wa kisiasa.
" Juhudi zao zimeimarisha amani kikanda, zimeboresha huduma za afya na elimu, pia zimeunda msingi imara wa utajiri wa kiuchumi na maendeleo ya rasilimali watu katika Africa". Amesema.
Aidha kwa upande wake Dk Jakaya Mrisho Kikwete amewashukuru waandaaji wa tuzo hizo na waafrica wote kwa ujumla na amesisitiza kuwa tuzo hiyo ni kwaajili ya waafrica wote , viongozi wa kisiasa, viongozi wa dini , majeshi ya ulinzi na usalama, watumishi wa umma , wakulima na wananchi wa kawaida wote .