Kutekwa Kwa Balozi Humphrey Polepole Jeshi La Police Tanzania Kufatilia Kwa Kina

Jeshi La Police Tanzania Kufatilia Kwa Kina Kutekwa Kwa Balozi Humphrey Polepole. 

Kutekwa Kwa Balozi Humphrey Polepole Leo

Pichani: Aliyewahi kuwa balozi wa Tanzania nchini Cuba Humphrey Polepole kabla ya kujiuzulu na kutenguliwa kwa uteuzi wake . 

Habari: Kufuatia uwepo wa habari za kutekwa kwa aliyekuwa balozi wa Tanzania nchini Cuba Humphrey Polepole usiku wa kuamkia leo tayari jeshi la police nchini Tanzania limetoa tamko juu ya habari hizo. 

Mapema siku ya leo jumatatu ya tarehe 06 October katika mitandao ya kijamii nchini Cuba kumezuka habari za kutekwa kwa Humphrey Polepole, habari zilizocharazwa mitandaoni na mtu aliyesema kuwa ni kaka wa Humphrey Polepole aliyejitambulisha kama Augustine Polepole.  

Baada ya uvumi wa habari hizo jeshi la police nchini Tanzania kupitia msemaji wake makao makuu ya jeshi hilo mjini Dodoma wametoa taarifa kamili isemayo kuwa '' Jeshi la police lingependa kutoa taarifa kuwa bado linaendelea kumsubiri ndugu Humphrey Polepole aripoti katika ofisi za mkurugenzi wa upelelezi makosa ya jinai, alitumiwa barua ya wito kwa mujibu wa sheria za nchi aripoti katika ofisi ya mkurugenzi wa upelelezi makosa ya jinai ili atoe maelezo kuhusiana na tuhuma mbalimbali alizozitoa kupitia mitandao ya kijamii lakini hadi leo hajatekeleza maelekezo hayo kwa mujibu wa sheria, jeshi la police limeona taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na ndugu zake kuwa ametekwa tayari tumeanza kufanyia kazi taarifa husika ili kupata ukweli wake " 


Next Post Previous Post
sr7themes.eu.org