Faida za kula carrot kila siku
Faida za kula carrot kila siku
Carrot ( karoti ) : Ni wazi kuwa unaifahamu vizuri karoti na mara kadhaa umekuwa ukisikia msikioni mwako kuhusu mzizi huu. Lakini pengine hukufanikiwa kufahamu kuhusu faida zake katika mwili na afya yako ,hivyo basi katika chapisho hili utafahamu kwa kina kuhusu faida za kula carrot kila siku katika maisha yako na afya pia .
Hata hivyo inakupasa ufahamu kuwa karoti zipo katika rangi tofauti, ukiachana na rangi ya orange zipo karoti zenye rangi ya zambarau, nyekundu na nyeupe . Umewahi kuona karoti za rangi hizi?
Tafiti mbalimbali zimefanywa kubaini faida za karoti katika afya na mwili wa binaadamu na kubaini virutubisho vilivyopo katika karoti ambavyo vinaweza kuboresha afya ya binaadamu katika kupambana na maradhi mbalimbali . Miongoni mwa tafiti hizo ni tafiti iliyochapishwa na shirika la maswala ya afya la health line. Tafiti ambayo imeweka bayana kuhusu virutubisho vinavyopatikana katika karoti.
Virutubisho vilivyopo katika karoti
- maji
- Sukari
- Vitamin K1
- Potassium
- Kambakamba ( fiber)
- Calories
- Fat
Vitamin na madini katika karoti .
Karoti imebeba idadi kubwa ya vitamin na madini , madini ambayo ni muhimu sana katika mwili wa binaadamu na afya yake pia. Miongoni mwa vitamin na madini hayo ni kama vile ;-
• Vitamin A; Karoti imejaa wingi wa Vitamin A, Vitamin A ni muhimu sana katika afya ya macho kwani husaidia kuona vizuri , kukua vizuri na huchochea kinga mwili .
• Vitamin K1; Vitamin K1 pia hupatikana katika karoti. Vitamin K1 ni muhimu sana katika afya ya mifupa .
• Potassium ; Potassium iliyopo katika karoti ni muhimu sana katika afya ya binaadamu, potassium husaidia katika kudhibiti shinikizo la damu .
• Vitamin B6; B6 iliyopo katika karoti husaidia sana katika mchakato wa kusharabu chakula mwilini .
Jee karoti hutibu na kuzuia maradhi gani?
- Hupunguza uwezekano wa kupata maradhi ya Saratani; Vyakula vyenye carotenoids kama karoti husaidia sana kuupa mwili uwezo wa kupambana na tezi za saratani , hususani saratani ya koo, utumbo na maziwa kwa wanawake .
- Huondoa na kutibu tatizo la ukavu macho ; Uwepo wa vitamin A katika karoti husaidia sana katika kuboresha afya ya macho na pia huongeza uwezo wa macho kuona kwa kuipa nguvu misuli ya macho .
- Hupunguza shinikizo la damu; Ulaji wa karoti kwa wingi husaidia sana katika kuondoa shinikizo la damu, ni wazi kuwa kupunguza shinikizo la damu husaidia sana katika kutibu maradhi ya moyo .
- Hupunguza uzito uliopitiliza ; Vyakula vyenye uchache wa calorie kama karoti husaidia sana katika kupunguza tatizo la uzito uliopitiliza .

