🚨Breaking News Ajali Ya Basi Na Teksi Yasababisha Vifo 11
Breaking News Watu 11 Wafariki South Africa Ajali Ya Basi Na Teksi Eastern Cape
South Africa: Watu wapatao 11 wanaripotiwa kufariki dunia kutokana na mgongano wa basi na teksi huko Eastern Cape. Ajali hiyo ya uso kwa uso imetokea jumapili ya leo mchana saa za Africa Kusini.
Habari kutoka South Africa zinaeleza kuwa ajali hiyo imetokea barabara ya R61 kati ya Flagstaff na Lusikisiki . Hata hivyo kwa mujibu wa shirika la usalama wa watumiaji wa barabara huko South Africa ( RTMC ) basi la City liner na Toyota Quantum ndio gari zilizogongana na kusababisha vifo vya watu hao kumi na mmoja waliokuwa katika toyota.
Aidha katika ajali hiyo majeruhi wote wamekimbizwa hospital za karibu na eneo la tukio kupatiwa matibabu na uangalizi.
Post a Comment