Header Ads

Djigui Diarra Ni Screen Protector Kweli

Djigui Diarra Aifuta Penalty Ya USMA Aokoa Mashambulizi Awa Man Of The Match Yanga Sc vs USMA CAFCC . 

Djigui Diarra Man Of The Match

Yanga Sc na Uongozi wake wanashauriwa na wadau mbalimbali na wapenzi wa soka la nchini Tanzania , kuhakikisha kuwa miongoni Mwa wachezaji wanaoendelea kuwepo Yanga Sc misimu yote basi ni huyu kijana kutoka nchini Mali Djigui Diarra . 

Watu wanamuita screen protector na mdaka mishale na jana katika mchezo wa fainali Yanga Sc vs USMA amethibitishia dunia kuwa yeye ni sawa sawa na majina anayoitwa. Mara baada ya kutangazwa kuwa man of the match Djigui Diarra alikuwa na haya ya kusema kupitia kurasa zake . 

Duka La Next Fashion Brand Jiunge Hapa Na Wewe

       " We have tried everything! We have tried everything! We gave it our all! We dreamed of it like crazy ! yes We deserved it like Kings but alas the man proposes God disposes, We will come back even stronger Inshallah by the grace of God. Big thank you to all " 

Ni ukweli usiofichika kuwa Djigui Diarra ni golikipa wa heshima, viwango na ubora sana na Yanga Sc bado inamuhitaji sana katika lango . Mbali na kuokoa magoli lakini pia huanzisha Mashambulizi, hupanga wachezaji wake na kuwaelekeza vizuri. 

Djigui Diarra ni mwenye kipaji kikubwa na Yanga Sc wamekuwa wakifanya vizuri sana kila wanapokuwa na golikipa huyu katika kila mchezo muhimu. Kuokoa mkwaju wa penalty si jambo jepesi, lakini kwa kijana Djigui Diarra imekuwa jambo rahisi katika mchezo mgumu na muhimu sana. 

Viwango vya golikipa huyu kutoka mali kwa mchezo wa jana vinatarajiwa kupaa zaidi na huwenda timu kadhaa za Africa zikahitaji saini yake kutaka kupewa huduma ya langoni, lakini Yanga Sc wanatakiwa kuhakikisha Djigui Diarra anabakia kwao. Hivyo Yanga Sc watakuwa katika kibarua kigumu cha kumlinda mdaka mishale huyu.

Djigui Diarra Yanga Sc vs USMA

Man of the match Djigui Diarra

Hakika Yanga Sc ni timu bora na wenye viwango, kucheza fainali kubwa na yenye ushindani kumeipa heshima Yanga Sc na Taifa la Tanzania kwaujumla. 

Powered by Blogger.