Picha Mandhari Ya Fukwe Za Mombasa Kenya

Picha Mandhari Ya Fukwe Za Mombasa 

Fukwe Za Mombasa nchini Kenya Leo

Mombasa: Pwani ya nchini kenya yenye fukwe nzuri, safi na kuvutia  pia . Wenyeji wakarimu na idadi kubwa ni waumini  wa dini ya kiislam . Vazi la stara kwa wenyeji wa mombasa sehemu ya utamudu wao. Khanzu  na Khanga ni sehemu ya vazi la utamaduni.

Umeshawahi kufika mombasa? Nini hutasahau kuhusu mombasa? basi kama tayari umewahi kufika au bado , modealer mwaandishi wa habari mbalimbali anakusogezea picha kadhaa za mandhari ya mombasa haswa pwani au baharini. 

Fukwe Za Mombasa Kenya Leo

Old port ni miongoni mwa kivutio kikubwa cha baharini ukiwa mombasa nchini kenya, ni kawaida kukuta watu wakifurahia eneo hili lenye  upepo mwanana wa bahari. 

Uvuvi mombasa kenya

Wavuvi na shughuli yao ya uvuvi ni miongoni mwa mambo utakayoshuhudia ukiwa katika fukwe za mombasa kenya. Ni kawaida sana kushuhudia wanaume wa rika tofauti wakiwa katika vyombo vya uvuvi wa baharini. Uvuvi huchangia pakubwa pato la wakazi wa mombasa. 

Ngamia Mombasa Kenya

Ngamia ni kivutio chengine utakachokiona ukiwa katika fukwe za mombasa. Ngamia ni sehemu ya mifugo inayopatikana ndani ya mombasa, ngamia huonekana sana katika fukwe za mombasa , ni jambo la kawaida kukutana na watu wakifurahi kupiga picha na ngamia katika fukwe za mombasa. 

Vazi la khanga Mombasa Kenya

Vazi la khanga ni kivutio chengine ukiwa katika fukwe za mombasa, khanga ni vazi la utamaduni wa watu wa pwani ya afrika mashariki. Vazi la khanga lina historia ndefu sana hapa africa mashariki, japo kwasasa vazi hili lililotapakaa kila kona lakini ni ukweli usiopingwa kuwa vazi hili asili yake ni pwani ya bahari ya hindi. Mombasa, Tanga, Zanzibar ni maeneo yenye historia ya vazi hili la khanga.  

Vazi la khanga Mombasa nchini Kenya

Kusafiri ni kujifunza vingi , kusafiri ni kuona yale ambayo eneo moja hayapo au kama yapo basi watu hufanya kwa tofauti moja au nyingine, unazijua ndifu? moja kuitwa moya jee ? basi vyote hivi utakutana navyo mombasa. Tukutane kwenye machapisho yajayo kwenye Cities Story session hapahapa