Bungeni Dodoma Kengele Ya Tahadhari Yawaondoa ukumbini wabunge

Kengele Ya Tahadhari Yawaondoa Wabunge Ukumbi Wa Bunge Dodoma . 

Kengele Ya Tahadhari Bungeni Dodoma

Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson ameahirisha kikao cha bunge kwa muda baada ya kengele ya dharura kulia kuashiria hatari. Hata hivyo amesema bunge litarejea baada ya dharura hiyo kutatuliwa. 

Aidha baada ya tukio hilo Spika Tulia Ackson amethibitisha kuwa chanzo cha kengele ya tahadhari ni uwepo wa vumbi katika alarm za tahadhari ya moto, na vumbi hilo limesababishwa na shughuli za ujenzi zinazoendelea katika majengo ya bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hivyo vumbi hilo limesababisha Kengele kulia ikihisi ni moshi.