Ulevi Wa Wazazi Kupindukia Watoto Huwa Walevi Mara Nne Ya Wazazi .
Madhara ya ulevi wa wazazi. Utafiti uliofanywa siku za hivi karibuni kuhusu vijana na afya ( Adolescence health ) na kisha kuchapishwa na jarida la habari la cnn umebainisha kuwa ulevi wa pombe uliokithiri wa wazazi husababisha watoto wao kuwa walevi wa kupindukia.
Katika utafiti huo wazazi walevi walifanyiwa utafiti na hatimae kugundulika kuwa hata watoto wao nao ni walevi na ulevi wa watoto wao ni mara nne ya ulevi wa wazazi. Sababu kubwa inayotajwa ya kwanini wazazi walevi kupindukia watoto wao huwa walevi mara nne yao ni kitendo cha wazazi walevi kushindwa kujizuia kuonekana na watoto wao wakiwa wamelewa.
Kitendo ambacho huwafanya vijana kuuona ulevi kuwa kitu cha kawaida, chenye kuzoeleka kwa wapesi na kisicho na dosari katika jamii. Ni kawaida sana katika jamii nyingi kukutana na walevi, walevi ambao nyuma yao kuna kundi la vijana ambao huwaita wazazi, mzazi ni sehemu ya kwanza ya mtoto kujifunza mtindo wa maisha na namna ya kuishi na wengine, hivyo inatajwa kuwa kama mzazi atakuwa na uwezo wa kunywa chupa za beer nane kwa siku kuna uwezekano wa mtoto wake kuja kunywa chupa za beer thelathini na mbili.