FBI Wamshikilia Mchungaji Pastor Jose Saez Kwa Kosa La Kushiriki Ngono Na Watoto.

Pastor Jose Saez Ashikiliwa Na FBI Kwa Kosa La Kushiriki Ngono Na Watoto Na Kusambaza Video Za Ngono Za Watoto . 


Federal Bureau Of Investigation ( FBI ) wanamshikilia pastor Jose Saez, Jr kwa kosa la kushiriki vitendo vya kingono na watoto pamoja na kusambaza video za ngono na watoto hao. 

FBI huko Long Island wamemtia kizuizini pastor Jose Saez Jr mara baada ya kupokea ujumbe mtandaoni ulioeleza bayana kuwa pastor huyo anajihusisha moja kwa moja na vitendo vya kingono na watoto. Habari zinaeleza kuwa mara baada ya maafisa wa FBI kufanya zoezi la kukagua walibaini video 15 za ngono katika simu ya pastor Jose Saez, video zilizokuwa zimehifadhiwa katika mtandao wa telegram.

Aidha moja ya video hizo inamhusisha mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka kumi na misita ( 16 ) akifanya ngono. Jose Saez baba wa watoto watatu amewaambia maafisa wa FBI kuwa alimuomba mtoto huyo kumtumia video hizo . Lakini hata hivyo pastor Jose Saez amekiri kwa maafisa wa FBI kuwa nikweli ameshiriki ngono na vijana wengine wengi na ameweka bayana kwa kusema kuwa watu wamsamehe kwani hawezi kuachana na vitendo hivyo 

Aidha pastor Jose Saez ni mchungaji huko Iglesia Cristiana Alumbrando El Camino Church. News 12 wameripoti . 

Tags