Duane Keefe D Davis Muuaji Wa Tupac Shakur Atozwa Faini Baada Ya Miaka 27.
Baada takribani miaka ishirini na saba (27) tangu kutokea kwa mauaji ya mwanamuziki wa hip-hop wa huko marekani Tupac Shakur, hatimae muuaji aburuzwa mahakamani kulipa juu ya mauaji yake.
Mnamo mwaka 1996 Tupac Shakur aliaga dunia kufuatia kupigwa risasi akiwa anaendesha gari huko Las Vegas marekani. Kifo na mauaji ya Tupac Shakur kimejaa simulizi na mambo mengi ya mauzauza , mbali na yote leo vyombo mbalimbali vya habari duniani kote vinaripoti kuhusu kuburuzwa mahakamani kwa Duane Keefe D Davis ambae ni muuaji wa Tupac.
Hatua hii imefikiwa baada ya matokeo ya uchunguzi ulioanza kufanywa tangu mwaka 1996 mara baada ya mauaji ya Tupac kutokea. Inaelezwa kuwa miaka yote hiyo familia ya Tupac Shakur ilikuwa ikiililia haki