Msitu Wa Amazon Hatarini Kukumbwa Na Ukame Zaidi Ya Watu 50,000 Wataathirika.
Brasilia: Habari kutoka nchini Brazil inaelezwa kuwa msitu wenye mvua nyingi wa Amazon upo hatarini kukumbwa na ukame mkali hadi ifikapo mwishoni mwa mwaka 2023. Habari zinaeleza kuwa kumekuwa na ongezeko kubwa la vifo vya samaki katika mito ya msitu wa amazon.
Kupungua kwa kasi kwa kina cha maji katika mito ya msitu wa amazon kumesababisha kuongezeka kwa idadi ya mizoga ya samaki inayoelea juu ya maji na kusababisha ongezeko la harufu mbaya kitu kinachopelekea kuongezeka kwa vifo vya samaki hao.
Ripoti zinaeleza kuwa inatarajiwa hadi kufikia mwisho wa mwaka 2023 takribani watu elfu hamsini waishio pembezoni mwa msitu huu mkubwa huko nchini Brazil watakuwa wameathiriwa na ukame huo .
Mamlaka za nchini Brazil zimethibitisha uwepo wa ukame huo unaosababishwa na kupungua kwa kina cha maji na kusababisha vifo vya samaki huku idadi nyingine ya samaki ikionekana kutapatapa katika maji mafupi bila matumaini ya kunusurika.
Picha zilizopigwa na shirika la habari la Reuters zinaonesha kundi kubwa la mizoga ya samaki hizo huko nchini Brazil.