Indonesia Kuiburuza Israel Mahakama Ya Kihalifu ( International Criminal Court )
Habari: Nchi ya Indonesia inaripotiwa kuwa imefikia uamuzi wa kuipeleka Israel katika mahakama ya kihalifu ya kimataifa ( international criminal court) ikiwa ni baada ya uvamizi wa Israel nchini Palestine kwa miaka 75.
Duru mbalimbali za habari zinaangazia kwa kina mzozo unaoendelea kati ya Israel na Palestine, mzozo ambao ni wa miaka mingi sana , lakini hata hivyo wanaharakati mbalimbali wa masuala ya kibinaadamu huko Palestine na mataifa mengine yanaunga mkono hatua iliyofikiwa na Indonesia ya kuiburuta Israel mahakamani.