Na mwaandishi wetu: Mataifa mbalimbali yameanza kukimbilia mahakama ya kihalifu ya kimataifa ICC kuishtaki Israel kwa mauaji ya kutisha ya raia wa Palestine tangu kuanza kwa mapigano dhidi ya Hamas.
Indonesia, Mexico, Chile na South Africa zimekuwa mstari wa mbele katika harakati hizi za kuipeleka Israel katika mahakama ya ICC. The Wall Street Journal inaripoti kuwa sababu kubwa ya Mexico na Chile kuungana kuipeleka Israel ICC ni kutokana na mauaji ya raia huko Gaza.
Katika ripoti ya habari kutoka nchini Mexico na Chile inasema kuwa mpango uliofikiww ni kuitaka ICC ifanye uchunguzi kubaini kuwa iwapo mashambulizi ya kuua raia wa Gaza yamefanywa na Israel na vikosi vyake kipindi cha operesheni ya kijeshi au ni Hamas ndio walifanya mauaji.