Malawi Kuzuia Mahindi Ya Tanzania.
Lilongwe: Nchi ya Malawi imeweka zuio la kuingia kwa zao la nafaka la mahindi kutoka nchini Tanzania kwa madai kuwa mahindi ya tanzania yamebainika kuwa na vimelea vya ugonjwa.
Shirika la utangazaji habari nchini Malawi Malawi Broadcasting limeripoti kuwa katazo hili ni muendelezo wa tangu 2012 ikiwa ni baada ya mahindi ya tanzania kubainika kuwa na ugonjwa wa Maize Lethal Necrotic.
Hata hivyo kupitia ukurasa wa mtandao wa X wa waziri wa kilimo nchini Tanzania imeripotiwa kuwa tayari mazungumzo kati ya pande mbili yamefanyika na kufikia muafaka na makubaliano ya pamoja. Waziri wa kilimo nchini Tanzania Hussein Bashe ameandika kuwa nchi ya Tanzania kwa upande wake imeruhusu magari ya maharage ya soya kutoka Malawi kuingia na shehena za mizigo katika mipaka ya nchini Tanzania.