Houthis Wapiga Bomu Na Kuharibu Nyaya Nne Za Optic Cable/ Fiber Red Sea .
Breaking News: Kikundi cha wapiganaji wa Houthis kinaripotiwa kuwa kimetekeleza mpango wake wa kupiga bomu na kisha kuharibu nyaya za fiber optic zilizopita chini ya maji ya bahari nyekundu ( Red Sea ) .
Habari zinaeleza kuwa kikundi cha Houthis kimeharibu nyaya nne mpaka sasa, aidha mchanganuo wa nyaya zilizoharibiwa ni AAE-1, Seacom, EIG, na TGN system cable. AAE -1 ni waya wa mawasiliano ya internet kati ya Asia mashariki hadi Europe kupitia Egypt, pia unaunganisha China upande wa Magharibi kupitia nchi ya Qatar na Pakistan, huku EIG ikimaanisha European Indian Gateway ukiunganisha Europe Kusini kupitia Egypt, Saudi Arabia, Djibouti, Dubai na India.
Kwa upande wa waya wa mawasiliano wa Seacom, nao umeharibiwa ambapo wenyewe huunganisha mawasiliano ya internet kati ya Europe, Africa, India na South Africa. Hata hivyo inatarajiwa kuwa nchi nyingi zitakazoathiriwa ni zile zilizopo maeneo ya Gulf . Bado mgogoro unaendelea athari kubwa zinaanza kujitokeza nini hatma?