Vituo Vya Police Chakavu Nchini Zimbabwe
Zimbabwe: Nchi ya barani Africa, nchi yenye idadi kubwa ya wasomi waliopata elimu ya juu katika vyuo vikubwa duniani ikiwemo oxford na hata Cambridge university. Hata hivyo Zimbabwe ni nchi yenye raia wachapa kazi kwelikweli lakini bado umaskini upo pale pale, shida iko wapi?
Pichani ni moja ya kituo cha police nchini Zimbabwe, kituo ambacho ni chakavu sana, nusu upande bati lipo na kisha upande mwingine hakuna bati kabisa ni mbao tupu. Mbali na uchakavu wa kituo hiki cha police habari kutoka nchini Zimbabwe zinaeleza kuwa hata hali ya muonekano wa magereza ya nchi hii ni mbaya sana.
Picha kutoka nchini Zimbabwe zinaripoti masikitiko makubwa waliyonayo wakina mama wajawazito katika moja ya wodi ya wazazi, hii ni baada ya uwepo wa kadhia ya kulala chini kutokana na ukosefu wa vitanda vya kulazia wagonjwa, shida ni nini nchini Zimbabwe?
Africa kulikoni? mbali na uwepo wa rasilimali mbalimbali zenye thamani kubwa lakini bado nchi nyingi za bara la Africa zimedidimia kwenye umaskini mkubwa au ndio usemi wa " kwenye miti hakuna wajenzi" ?