South Africa Waliomuua AKA Wafikishwa Mahakamani Nchini South Africa Leo .
South Africa: Washukiwa na watuhumiwa wa mauaji ya mwanamuziki AKA nchini South Africa leo hii wamefikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza tangu kutokea kwa mauaji ya msanii huyo pamoja na rafiki yake.
Mara baada ya watuhumiwa hao kufikishwa mahakamani leo hii , muendesha mashaka wa mahakama aliwaomba kuvua mask walizokuwa wamevaa ili waweze kuonekana sura zao. Hata hivyo kati ya watuhumiwa saba ni watuhumiwa watano tuu ndio ambao majina yao yameweza kufahamika mpaka sasa ambao ni Lundokuhle Thabani Mkhwanazi (30), Lindani Zenzele Ndimande (35), Siyanda Eddie Myeza (21) , Mziwethemba Harvey Gwabeni (36) na Lundokuhle Lindo Ndimande (29).
Hata kesi ya watuhumiwa hao imesogezwa mbele na mahakama hadi mnamo tarehe 6, 14, 19 na 27 ya mwezi march mwaka 2024. Mara baada ya kesi kusogezwa mbele waandishi wa habari waliokuwa nje ya mahakama walipata nafasi ya kumhoji baba mzazi wa AKA kuhusu iwapo anahisi kuwa watuhumiwa waliokamatwa ndio wauaji wa mtoto wake ? Hata hivyo baba mzazi huyo alisema kuwa yeye hana uhakika anaiachia mahakama kwa uchunguzi zaidi.