FAHAMU KUWA MCHWA HULALA NAO .
Bila shaka umewahi kusikia umaarufu wa mdudu mchwa kama kiumbe na mdudu ambae huwa busy muda wote kwa shughuli za ujenzi wa vichuguu ( makazi ) yao, lakini huwenda hukuwahi kusikia kamwe kuhusu muda wao wa kulala na kupumzika na hata muda wao wa kuishi duniani.
Utafiti uliofanywa na James & Cottel miaka kadhaa iliyopita imebainika kuwa mchwa hulala na kupata muda wa kupumzika kama binaadamu au viumbe wengine. James & Cottel katika utafiti wao wamebaini kuwa mchwa hupumzika yaani kulala kwa dakika nane ( 08 ) pekee ndani ya saa kumi na mbili kwa siku .
Utafiti wa James & Cottel unaenda mbali zaidi hadi kubainisha muda wa kuishi wa kiumbe mchwa katika dunia kuwa ni miezi miwili, nane , kumi na mbili na hata miaka miwili kutokana na aina pamoja na majukumu ya mchwa katika makazi yao . Mfano inatajwa kuwa mchwa dume hufa mara moja baada ya kumpanda mchwa jike.
Lakini mchwa malkia baada ya kupandwa huweza kuishi kwa kipindi kirefu cha muda hadi kufikia miaka miwili au zaidi ya hapo. Hata hivyo mgawanyo wa kazi na majukumu ya mchwa katika makazi yao hufanana sana na mgawanyo wa kazi wa wadudu nyuki, vilele inampasa kila mchwa kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa sana vinginevyo anaweza kuawa.
Jukumu kubwa, gumu na zito katika majukumu yote ya mchwa huwenda ikawa ni kumlinda malkia wao na kujenga makazi yaani vichuguu. Vichuguu hujengwa usiku na mchana huku muda wa kupumzika ukiwa mchache na mfinyu sana . Na hayo ndio usiyoyajua kuhusu mdudu mchwa.