Ahmed Shabiby Na Shabiby Line Kushusha Bus Mpya

Shabiby Bus Mpya Za Kisasa Yutong D-14. 

Shabiby Busy Mpya Yutong D-14

Dodoma: Kampuni ya usafirishaji abiria yenye makao yake mjini Dodoma Shabiby Line inayomilikiwa na Ahmed Shabiby imetangaza ujio wa bus zake mpya kabisa. 

Kupitia ukurasa wa Instagram wa kampuni hiyo ya usafirishaji imesema kuwa bus hizo ni aina ya Yutong D-14 ambazo ni za kisasa. 
Mnamo October 29 kampuni ya usafirishaji abiria ya Shabiby ni miongoni mwa zilizoathiriwa kwa kuchomewa moto baadhi ya magari yake . 

Ni siku chache zimepita tangu kadhia na adha hiyo kutokea, takribani siku kumi tuu zimepita na sasa Shabiby inatangaza ujio wa gari zake mpya kabisa kuendelea kutoa huduma ya usafirishaji abiria nchini Tanzania kutoka Dar es salaam kwenda Dodoma na mikoa mingine. Usafiri wa umma wa mwendokasi umesimamisha huduma lakini Shabiby anarejea kwa kishindo kikubwa. 
Previous Post
sr7themes.eu.org