Mahakamani Kisutu Leo Niffer Afikishwa Kusomewa Mashitaka

Mfanyabiashara Niffer Afikishwa Kusomewa Mashitaka Mahakamani Kisutu Leo. 

Niffer mahakamani Kisutu Leo

Dar es salaam: Mfanyabiashara na mwana mitandao wa nchini Tanzania Jennifer Jovian maarufu kama Niffer leo November 07 amefikishwa mbele ya mahakama ya hakimu mkazi kisutu jijini Dar es salaam kusomewa mashitaka yanayomkabili. 

Mnamo October 27 Niffer akiwa dukani kwake alikamatwa na jeshi la police nchini Tanzania kwa kosa la kuchochea vurugu na maandamano yaliyopangwa kufanyika siku ya uchaguzi mkuu October 29 mwaka huu . 

Habari kutoka mahakamani Kisutu jijini Dar es salaam zinaeleza kuwa Niffer anakabiliwa na kesi ya uhaini. Katika watu wake wa karibu waliohudhuria mahakamani hapo leo ni mama yake mzazi Aisha Izaak kusikiliza shauri la kesi ya mtoto wake huyo ambae tangu October 27 alikuwa akishikiliwa na jeshi la police. 
Next Post Previous Post
sr7themes.eu.org