UPDATE 🔴: AACHWA KWA KISIRANI CHA MIMBA.
Wilayani Pangani mkoani Tanga. Binti umri wa miaka 24 mkazi wa wilayani humo yamemkuta makubwa baada ya kuachwa akiwa na ujauzito wa miezi mitano .
Binti huyo ambae ameomba jina lake lihifadhiwe ameeleza kuwa hajui sababu kubwa ni nini . Hata hivyo binti huyo amethibitisha kuwa kisirani (Gubu ) la mimba ndio huwenda ikawa sababu ya kuachwa kwake.
" Kabla ya ujauzito sikuwa hivi , siku moja nilihitaji aninunulie tambi nipike hakuwa na pesa , nilikasirika sana na kupasua vikombe vyote kabatini. Lakini siku moja alikuja na rafiki zake nyumbani simu yake iliita na nilisikia sauti ya msichana akiongea nae ndipo nilipoikamata simu na kuipasua . .."( Maelezo ya bint huyo )
Binti huyo amethibitisha kuwa kuachwa kwake ni kutokana na mume wake kuchoshwa na visa vyake kipindi hiki Cha ujauzito. Ni zaidi ya mara mbili binti kupasua simu za gharama za mume wake.
Baada ya reporter wetu kufanya mazungumzo na mume wa binti huyu imebainika kuwa nikweli mume amemuacha mke wake huyo kwa talaka tatu kwa mujibu wa dini yao .
"Sitamani kabisa kumrudia ,ni jeuri sana na mwenye kiburi. Alikuwa anatafuta sababu siku nyingi sana, nilivumilia lakini sasa nimechoka , Nina kila sababu ya kumuacha . Ujauzito nitatunza kama kawaida...." ( Mume)
Je unafikiri nani alaumiwe?
Tuandikie comment yako hapa tutaisoma
Post a Comment