UPDATE 🔴: DAMIAN SOUL ACHARUKWA TUZO HAZINA WELEDI.
Habari Kamili
Msanii wa kizazi kipya nchini Tanzania DAMIAN SOUL . Ameweka wazi kupitia ukurasa wake wa instagram kuwa hakupendezwa kabisa na nafasi aliyochaguliwa kuwania katika tuzo za TMA .
Damian Soul hitsong maker wa Mapopo na ambae yupo muda mrefu katika soko la Music nchini Tanzania amepangwa katika category ya msanii bora chipukizi tuzo za TMA. Hata hivyo DAMIAN SOUL ameandika kuwa Tuzo za TMA hazizingatii weledi wala kufanya uchunguzi wowote.
Mbali na hayo DAMIAN SOUL mpaka kufikia jioni hii tayari amejitoa katika kuwania tuzo hizi kutokana na category aliyowekwa (Msanii bora chipukizi) hali ya kuwa yupo katika soko la music muda mrefu.
Hata hivyo mapema leo hii habari mitandaoni zilizuka habari kuwa huwenda label ya Wasafi wamejitoa katika kuwania tuzo hizi.
Kuwa karibu na modealer.
Post a Comment