UPDATE 🔴: WILL SMITH KUJIUZULU
Summary
Will Smith amejiuzulu uanachama katika film academy . Amesema kuwa ameumizwa sana na amevunjika moyo sana . Ameyasema hayo siku ya jana (ijumaa) .
April 01, 2022 (siku ya ijumaa) . Shirika la habari la Reuters limeripoti kuwa muigizaji maarufu Will Smith amejiuzulu uanachama wake Hollywood academy of motion picture, arts and science.
Will Smith amejiuzulu uanachama siku ya jana na amesema kuwa kofi alilompiga presenter Chris Rock jukwaani mwaka huu kwenye Oscar lilikuwa la kushtukiza na lenye maumivu sana .
" Nimesaliti uaminifu wa academy , nimedhalilisha washiriki wengine na washindi kwenye nafasi zao kushereheka na kusherehekewa . Nimeumizwa sana moyoni , hivyo najiuzulu uanachama kwenye ya motion picture, arts and science na nitakubaliana na matokeo yoyote ambayo bodi itachukua " Alisema .
Hata hivyo mapema leo hii inaelezwa kuwa academy imethibitisha kupoke barua kutoka kwa Will Smith akiomba kujiuzulu uanachama wake katika academy ya motion picture, arts and science .
Kuuzwa kwa picha ya Will Smith
Tovuti maarufu ya uuzaji picha duniani mapema wiki iliyopita imeiingiza picha ya Will Smith aliyompiga kofi jukwaani Chris Rock katika mauzo . Ikumbukwe kuwa Will Smith alimpiga kofi Presenter Chris Rock baada ya kumtania mke wa Will Smith kutokana na kipara chake . Picha hiyo inauzwa kwa bei tofautitofauti kutokana na ukubwa tofautitofauti pia . Ahsante kwa kuwa sehemu ya wasomaji wetu. Tafadhali kuwa karibu nasi.
Post a Comment