Header Ads

BREAKING NEWS 🔴:IGP SIRRO ATOA POLE SAKATA LA PANYA ROAD

   IGP SIRRO ATOA POLE KUNDUCHI 

                     Watch this video 

Summary:  

IGP SIRRO amewatembelea waliojeruhiwa na kundi la Uhalifu la panya road kunduchi dar es salaam. Awataka vijana wa panya road kuacha mara moja kwa usalama wa maisha yao .

Mkuu wa jeshi la police nchini Tanzania IGP SIMON SIRRO hapo jana amewatembelea waliojeruhiwa na genge la kihalifu la panya road kunduchi dar es salaam na kuwapa pole . Kitendo hiki Cha kiungwana kimefanyika jana sambamba na hayo SIRRO ametoa onyo kali kwa vijana wa panya road kwa kuwataka waache mara moja kwa usalama wa maisha yao .

"Panya road nawapa salamu .....kama unataka maisha yako yawe vizuri acha hiyo.....kama ulikuwa na panga lako nenda kalitupe mahala pengine..." IGP SIRRO.

Mapema mwanzoni mwa wiki hii vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania vililiripoti kutokea kwa tukio la watu kujeruhiwa na kikundi cha panya road kunduchi dar es salaam. 


No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

Powered by Blogger.