Header Ads

HAKUNA BIASHARA YA KUUZA VIDOLE ZIMBABWE

 NAIBU WAZIRI WA HABARI ZIMBABWE ATHIBITISHA KUWA NI UZUSHI .



Summary: "Tulifanya utafiti juu ya suala hili na tukagundua kuwa ni uongo. Ni taarifa za mitandao ya kijamii zinazolenga kuchafua jina la nchi.." Alisema Paradza.

Naibu Waziri wa habari nchini Zimbabwe Kindness Paradza amekanusha madai ya kuwa wananchi wake wanauza vidole vyao vya miguu ili kupata utajiri .

Baada ya uvumi na tetesi kuzagaa kwenye mitandao ya kijamii juu ya uwepo wa biashara ya uuzaji viungo huko nchini Zimbabwe leo naibu Waziri wa habari wa nchi hiyo amekanusha .

Hata hivyo ameongeza kuwa habari hizo zinaenezwa na watu wenye nia ovu na nchi ya Zimbabwe. Mapema leo hii gazeti la The Herald limeandika kuwa mtu anayedaiwa kuhusika na biashara hiyo amekiri kuwa wakati anatoa tamko la kuhusika na biashara hii alikuwa amelewa .

Ikumbukwe kuwa siku kadhaa zilizopita habari kuhusu uwepo wa biashara ya kuuza vidole nchini Zimbabwe ilishika hatamu huku baadhi ya watu wakieleza kuwa sababu kubwa ya kuibuka kwa biashara hii ni ugumu wa maisha unaosababishwa na hali ngumu ya kiuchumi nchini humo. Hata hivyo baadhi ya watu wameeleza kuwa sababu ya kuibuka kwa biashara hii ni imani za kishirikina .

Video kadhaa zinasambaa mtandaoni zikionyesha watu wakikatwa vidole na kisha kupewa fedha nyingi sana na magari .  

(Truthful) <<<

No comments

Note: only a member of this blog may post a comment.

Powered by Blogger.